Numbers 15:32-36

Mvunja Sabato Auawe

32 aWaisraeli walipokuwa jangwani, mtu mmoja alikutwa akikusanya kuni siku ya Sabato. 33Wale waliomkuta akikusanya kuni wakamleta kwa Mose, Aroni na kusanyiko lote, 34 bnao wakamweka kifungoni, kwa sababu haikufahamika kwa wazi kwamba afanyiwe nini. 35 cNdipo Bwana akamwambia Mose, “Huyo mtu ni lazima afe. Kusanyiko lote lazima limpige mawe nje ya kambi.” 36 dHivyo kusanyiko likamtoa nje ya kambi na kumpiga mawe hadi akafa, kama Bwana alivyomwamuru Mose.

Copyright information for SwhNEN